UJASIRIAMALI.
kumekuwa na mitazamo na tafsiri nyingi kuhusu ujasiriamali,wengi hudhani kuwa ujasiriamali ni kumiliki duka,kuwa na biashara.nk.wengine hufikiri ni kuwa na ujuzi wa kutengeneza vitu kama vile sabuni,madawa ya kufanyia usafi na vitu vingine kama hivi.Vitu vyote nilivyovitaja hapo havitoshi kutoa tafsiri ya mjasiriamali.ujasiriamali waga haufundishwi bali ni tabia ya mtu ndiyo humfanya awe mjasiriamali.kitu kinachosemekana kuwa ni mafunzo ya ujasiriamali kimsingi siyo ujasiriamali bali huwa yana lengo la kutafuta masoko ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali,mfano kama nilivyotangulia kusema watu wanaofundishwa kuchanganya kemikali kwa ajiri ya kupata sabuni huu siyo ujasiriamali bali ulenga kumpa fulsa pana mzalishaji wa kemikali husika ili kupanua soko lake, kimsingi yeye ndiye tunaweza kumwita mjasiriali na hawa wachanganyaji tunaweza kuwaita wachuuzi kwasababu huwa wanatengeneza hizo sabuni majumbani kwao na mara nyingi ulazimika kuwa katika vikundi ili kuimalisha uwezo wao wa k...