UJASIRIAMALI.
kumekuwa na mitazamo na tafsiri nyingi kuhusu ujasiriamali,wengi hudhani kuwa ujasiriamali ni kumiliki duka,kuwa na biashara.nk.wengine hufikiri ni kuwa na ujuzi wa kutengeneza vitu kama vile sabuni,madawa ya kufanyia usafi na vitu vingine kama hivi.Vitu vyote nilivyovitaja hapo havitoshi kutoa tafsiri ya mjasiriamali.ujasiriamali waga haufundishwi bali ni tabia ya mtu ndiyo humfanya awe mjasiriamali.kitu kinachosemekana kuwa ni mafunzo ya ujasiriamali kimsingi siyo ujasiriamali bali huwa yana lengo la kutafuta masoko ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali,mfano kama nilivyotangulia kusema watu wanaofundishwa kuchanganya kemikali kwa ajiri ya kupata sabuni huu siyo ujasiriamali bali ulenga kumpa fulsa pana mzalishaji wa kemikali husika ili kupanua soko lake, kimsingi yeye ndiye tunaweza kumwita mjasiriali na hawa wachanganyaji tunaweza kuwaita wachuuzi kwasababu huwa wanatengeneza hizo sabuni majumbani kwao na mara nyingi ulazimika kuwa katika vikundi ili kuimalisha uwezo wao wa kuzalisha bidhaa yao.Hawa wachuuzi ufanya kazi zao mara nyingi huwa hawajui soko lao liko wapi hivyo huishia kugawana bidhaa ili kusaka masoko na pengine hulazimika kuzinunua wao wenyewe,kosa wanalolifanya wajasiriamali wa namna hii ni kuingia kwenye uzalishaji bila kujiuliza maswali kama haya;soko langu liko wapi,wateja wangu ni akina nani,washindani wangu ni akina nani,nifanye kitu gani cha tofauti ili kukabiliana na washindani wangu katika soko.Bila kujiuliza maswali kama hayo utaishia kuuza kwa bahati tu na bidhaa yako haiwezi kuwa na kasi nzuri na hii ndiyo humtofautisha mjasiriamali na mchuuzi.
Sasa turudi kwenye mada yetu kujua mjasiriamali ni mtu wa namna gani,kama lilivyotangulia kusema ujasiriamali ni tabia na kwa maneno mengine tunaweza kuuita utamaduni ambao mtu anauishi,ujasiriamali siyo jambo la kuamka leo na kusema nataka kuwa mjasiamali,kinachomfanya mtu aitwe mjasiriamali ni zile sifa au tabia za msingi za ujasiriamali.Ebu sasa tuzichambue hizo sifa au tabia zinazomfanya mtu aitwe mjasiriamali;
1)mjasiriamali ni lazima awe na maono;maono ni ile hali ya kutaza fulsa zilizopo au kuibua fulsa nyingine za kutoa huduma ili kutatua tatizo lililomo katika jamii,hii ni hali ya kujenga picha kubwa unataka kufanya nini bila kujiuliza utafikiaje lengo lako wala kujiuliza utapataje mtaji.
2)Uthubutu;Mjasiriamali lazima awe na uthubutu,na ujasiri wakuanzisha mambo bila ya kukatishwa tamaa na changamoto zinazoweza kutokea kabla ya kuanza,wakati wa utekelezaji na baada ya utekelezaji,mjasiriamali ata akishindwa kufikia malengo kamwe huwa habadilishi malengo yake bali ujipanga upya kwa kubadiri mikakati ili kufikia malengo.
3)kuwa na mahusiano na watu wengine;mjasiriamali ni lazima kuwa na mahusiano na watu wengine na nilazima aamini katika uduma anayoitoa na kuweza kuwashawishi wateja wake wanunue bidhaa zake au watumie huduma zake,lazima pia uweze kujenga mahusiano mazuri na wateja wako pia ni lazima uwe na uwezo wa kupata mrejesho na kutatua changamoto zinazoletwa na wateja wako.
Comments
Post a Comment