ujuzi katika ujasiriamali
Ili uweze kuwa mjasiriamali bora ni lazima utumie ule ujuzi wako ambao unakutofautisha na watu wengine,kila mtu aliumbwa akiwa na ujuzi au vipawa vya pekee ila ni watu wachache wanaoweza kugundua vipawa vyao na kuanza kuvitumia kikamilifu katika harakati za kujiletea mafanikio.Watu wengi usubiri mtu wa kuwatengenezea njia au kuonyesha kitu fulani kwa vitendo kuwa kinawezekana ndipo nao wachukue atua kwa kuiga shughuri au ujasiriamali anaofanya mwenzao.
Watu wengine utegemea sana wahamasishaji ili kuweza kupata hamasa na kuchukua hatua lakini ile hamasa huwepo kwa kitambo na kisha hupotea bila kufanyiwa kazi
Kitu cha muhimu ili ujuzi wako wa asili uweze kutumika ni kuchukua hatua bila kujari vikwazo vyovyote vinavyojitokeza,pia kuhepuka kuhairisha mambo kwa sababu mbali mbali
Comments
Post a Comment