MBINU ZA KUBUNI NA KUENDESHA UJASILIA WENYE KUKULETEA MAFANIKIO

Kuna njia nyingi za kufanya ujasiria mali,lakini ili uweze kufanikiwa unaitaji kuzingatia mambo kadhaa.

1)Kwanza kabisa unatakiwa kuwa mbunifu wa mambo mapya ambayo hayajawai kufanywa na mtu yeyote au kufanya mambo ambayo tayari yanafanywa na watu wengi lakini kwa njia tofauti,mfano;unaweza kugundua njia bora zaidi ya kuzalisha nishati ya umeme,hili litakuwa ni wazo jipya kabisa nalinaweza kutumiwa na jamii ili kuweza kujipatia umeme wenye gharama nafuu na usiyokuwa na hathari kwa mazingra.mfano mwingine ni kufanya mambo ambayo tayari watu wengine wanafanya ila kwa njia tofauti mfano,ukibuni kutengeneza mapambo kama yale yanayotoka china na ukayatengeneza kwa ubora kama hule hule wa kichina au zaidi,hii itatasaidia mtandao wa bidhaa yako kuleta changamoto kwa bidhaa hiyo ya kichina na kuifanya nguvu ya soko kwa bidha yako kuwa kubwa zaidi.

2)Kujiamini;mjasiriamali ni lazima kujiamini na kuhepuka kukatishwa tamaa kutokanako na mazingira pamoja na watu wanaokuzunguka.Hepuka kuhairisha hairisha mambo kwa woga wa kushindwa kwani hii usababisha mipango mizuri ya wajasiriamali kubaki kwenye makarata au kwenye vichwa vyao bila kufanyiwa kazi.Kwenye hali kama hii wajasiriamali ubaki katika mashaka kwa sababu ile roho ya kijasiriamali uendelea kuziambina nafsi zao kuchukua hatua,wakati mwingine usababisha msongo wa mawazo na kuwafanya wajasiriamali wengi kujiona wanyonge na wenye kukata tamaa.

3)kutumia rasilimali zilizopo;rasilimali ni vitu watu pamoja na pesa,huwezi kuendesha shughuri yoyote bila kuwa na rasilimali,wajasiriamali mahili ulenga kutumia rasilimali zinazoweza kupatika kwa ulahisi katika mazingira yao na kwa gharama nafuu,mfano kama unatengeneza shanga unaweza kuamua kutumia vitu vinavyopatikana kwa ulahisi katika mazingira unamoishi ama vile chupa tupu za maji,mabaki ya vipande vya mbao na miti,mifupa ya wanyama nk

4)Ubunifu wa teknologia;hii ukiiangali kwa haraka unaweza kufikiri  inafanana na namba moja,hapana huu ni ubunifu wa utaalamu unaoweza kutumia rasiriamali kufanikisha utekerezaji uliyomo kwenye kipengere namba moja.Wajasiria mali wengi ukwamia hapa pia,kwa kujihisi kuwa hawana uwezo wa kubuni teknologia ya aina yoyote au kuhisi kuwa hizo teknologia zinaweza kutumia gharama kubwa sana.

5)Kuwa na roho ya kijasiriamali;Ili kukamilisha mafanikio yako wewe kama mjasiriamali unatakiwa kuwa na tabia za kijasiriamali,unatakiwa kuamini kuwa ujasiriamali siyo kumiliki duka,au biashara bali ni kusababisha mambo yatokee ili kuboresha hali ya maisha kwa ujumla

Comments

Popular posts from this blog

ujuzi katika ujasiriamali

UJASIRIAMALI.