MTAJI

Je,unajua kuwa unaweza kuanzisha biashara au ujasilia mali kwa mtaji mdogo au bila mtaji wowote wa pesa?kama jibu ni hapana,hapa ndo sehemu sahihi ya wewe kujifunza mbinu na hatimaye kuelewa jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yako kwa mtaji kidogo au bila mtaji wowote wa fedha.Najua haitakuwa lahisi kwako kuamini hivyo,ila kadri tutakavyoende kujifunza utaelewa na kama ukiyaweka yote tutakayojifunza,sina shaka utafanikiwa katika mipango yako ya biashara.
    Unapoongerea mtaji kwa mtazamo wa kawaida watu ufikiri kuwa ni pesa tu,ata mimi mwenyewe niliamini hivyo mwanzani,lakini baada ya kujifunza nilianza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu mtaji.Sisemi kuwa pesa siyo mtaji,hapana namaanisha kuwa pesa ni sehemu tu ya mtaji na haina umuhimu sana katika mtaji.
Sasa tuone sehemu muhimu ya mtaji ni hip? Kwa ufupi sehemu kuu ya mtaji ni wazo la kutumia vitu tulivyo navyo katika mazingira yetu kupitia teknologia lahisi ambazo pia ubiniwa na wajasilia mali.Hii haiitaji pesa bali ni ubunifu.Nitatoa mfano kuna mjasiliamali alianza kutumi vitu vya kawaida sana vinavyopatikana katika mazingira yetu ya kila siku vitu hivyo ni kama:vyuma,makopo ya plastic magurudu ya magari yaliyokwisha matumizi,mabaki ya vitambaa n.k..Ameweza kuunda vitu mbali mbali na kuviuza,sasa hivi amepata pesa ya kutosha na tayari anamiliki biashara,tunaweza kusema ni mfanya biashara ya kati.
   Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, tusitegemee pesa tu kama mtaji wa biashara kwa sababu kama hatuna wazo zuri la kufanyia kazi tutakumbana na changamoto katika masoko ya bidhaa na huduma na hivyo kuanguka kibiashara.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUBUNI NA KUENDESHA UJASILIA WENYE KUKULETEA MAFANIKIO

ujuzi katika ujasiriamali

UJASIRIAMALI.